Mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, aliyefahamika kwa jina moja la Jafari, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akitibia kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na kifua.
Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008.
Wakati kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini.
Ratiba kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa huenda msiba huo ukawa maeneo ya Chaline au Lugoba ambako ni nyumbani kwa wazazi wa Marehemu.
0 COMMENTS:
Post a Comment