Roberto MartÃnez amesaini dili ya miaka mine kuinoa Everton. Martinez aliyekuwa kocha wa Wigan ameingia mkataba huo na tayari Everton imethibitisha kwamba ndiye mrithi wa David Moyes aliyejiunga na Manchester United.
Martinez aliipa Wigan ubingwa wa Kombe la FA kwa kuinyoa Man City katika fainali lakini siku chache baadaye wakafungwa na Arsenal bao nne na kushuka daraja.
Rais wa Everton, Bill Kenwright amethibitisha kwamba Martiney ndiye kocha mpya wa timu hiyo maarufu kama The Toffees.
0 COMMENTS:
Post a Comment