June 25, 2013



Katibu Mkuu wa Baraza la Soka la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholas Musonye amesema michuano ya Kombe la Kagame inafanya vizuri zaidi.

Musonye amesema michuano hiyo imekuwa na mafanikio makubwa tofauti ilivyotarajiwa na wengi hasa baada ya kuwa na matatizo lukuki.
Akizungumza kutoka Kharthoum, Sudan, Musonye alisema michuano hiyo sasa imefikia katika hatua ya robo fainali na bado idadi kubwa ya watu inajitokeza.

“Cecafa tunasikia raha sana kutokana na idadi kubwa ya watu inayojitokeza katika mechi zetu. Hakika ni kitu cha kijivunia,” alisema na alipoulizwa kujitoa kwa timu za Tanzania hakujaathiri kitu, alijibu.

“Sitaki kuzungumzia kuhusiana na timu za Tanzania, lakini niamini kwamba mambo yanakwenda vizuri sana.”

Michuano hiyo, kesho inaanza kutimua vumbi katika hatua ya robo fainali kuwania kucheza nusu fainali.

Simba, Falcon ya Zanzibar na waliokuwa mabingwa watetezi Yanga walitangaza kujiondoa katika michuano hiyo kutokana na kuhofia usalama, uamuzi uliomuudhi kupita kiasi Musonye.
Timu nyingine iliyojitoa ni mabingwa wa Kenya, Tusker ambayo pia ilitangaza kuhofia usalama.

Mpango mzima wa robo fainali uko hivi:
 JUMATANO:
APR Vs Express
Rayon Vs URA
ALHAMISI:
Vital’O Vs Ports Djibout
El Shandy Vs El Merreikh

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic