Pamoja na kukaa nje bila ya kupata namba kwa zaidi ya miezi mitano sasa,
mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ameanza kazi.
Okwi raia wa Uganda alicheza kuanzia mwanzo katika mechi kati ya timu yake
ya Etoile du Sahel dhidi ya JSMB.
Katika mechi hiyo ya ligi Okwi hakufunga lakini ndiye aliyekuwa nyota
kutokana na usumbufu mkubwa aliowapa mabeki wa timu pinzani.
Hadi mechi inaisha alifanyiwa faulo 17 na alitoa pasi ya bao ikiwa ni
pamoja na kusababisha faulo ambayo baadaye iilizaa penalty.
Mabao ya Etoile yalifungwa na Mossaab Sassi katika dakika ya 26 na Jaziri
katika dakika ya 81 na kupa ushindi Etoile wa mabao 2´-1 huku bao la wageni
likifungwa na Med Derrag katika dakika ya 43.
Tokea ametua Tunisia, Okwi alikuwa akiwekwa benchi ingawa alishiriki
mazoezi kama kawaida.
Awali ilionekana kama kutaka kumkatisha tamaa Mganda huyo lakini sasa
anaonekana kupata uhakika wa namba.
Hata kama hatacheza, lakini kocha lazima atakuwa anamtupia jicho hasa
kutokana na uwezo aliuonyesha katika mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment