Na Saleh Ally, Frankfurt
REAL Madrid ni kati ya timu zinazosifiwa kuwa na utaalamu mkubwa katika
masuala ya masoko.
Wakali hao, tayari wameanza kuuza jezi zao mpya zizakazotumika katika msimu
ujao.
Katika miji mitatu ambayo Salehjembe imetembelea kwa siku tano tayari kuna
jezi za Real Madrid zenye chata ya Fly Emirates.
Wakati Madrid wameanza kuuza jezi mpya, wenyeji kama Borussia Dortmund na
mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich bado wamelala.
Maduka mengi ya michezo kama Freiburg, Wiesbaden na hapa Frankfurt tayari
yana uzi huo mpya wa Madrid.
Katika maduka hayo, bado jezi ya timu za Ujerumani zinazouzwa ni zile za
msimu uliopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment