Mshauri wa
ufundi wa kamati ya maandalizi mbio za Tabora Marathon, Tullo Chambo
ameishukuru kampuni ya simu ya Vodacom kwa msaada wa fulana 100 zilizotolewa
jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake alisema kuwa Vodacom imekuwa msaada mkubwa kwao kwa
kuwezesha upatikanaji wa fulana hizo ambazo zitatumika siku ya tukio juni 22.
“Tunaishukuru
kampuni ya mawasiliano ya simu ya vodacom kwa msaada huo we fulana na
tunategemea kuendelea kushirikiana nao hapo baadaye,” alisema Chambo
Akielezea
maandalizi ya mbio hizo zitakazofanyika
mwishoni mwa wiki hii, Chambo alisema kuwa hivi sasa wako kwenye hatua za
mwisho ambapo mbio hizo zitakuwa ni za kilometa 21 kwa wanaume,16 kwa wanawake
pamoja na kilometa tano kwa watoto na watu wa umri wa kati.
Akikabidhi fulana hizo kwa niaba ya kampuni yake Matina Nkurlu
ambaye ni meneja mahusiano
alisema kwa kutambua umuhimu wa
michezo nchini ndiyo sababu kubwa iliyowasukuma kutoa udhamini wa fulana 100
kwa ajili ya mashindano hayo .
“Vodacom
Tanzania itaendelea kudhamini na
kuboresha michezo hapa nchini ikiwa ni wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara na pia jamii inapaswa kutambua kuwa kampuni
hii ni kwa ajili ya watanzania”Alisema Nkurlu.
Mbio za
tabora marathon zinatarajiwa kufanyika mkoani Tabora Jumamosi ya juni 22 ambapo
Vodacom ni kati ya wadhamini wa mbio hizo, Filbert Bay Foundation, NGF Company Limited.
Kampuni ya
mabasi ya NBS, Emmanuel Mwakaataka
pamoja na Sarah Ramadhani ambaye
ni makamu mstaafu wa Rais Chama cha Riadha
Tanzania (RT).
0 COMMENTS:
Post a Comment