Nimetua nchini Ujerumani, kwanza
ninaanza na vijana wa Kitanzania ambao wako katika project maalum ya Fels na
wanaendelea kujifunza mambo mengi, tutakuwa tunataarifiana kiana.
lakini bado naendelea na kozi fupi
kuhusiana na soka la Ujerumani na nini kimefanya liendelee kuwa imara zaidi kwa
miaka mingi huku msimu huu likitesa zaidi.
Ninapita katika klabu kadhaa zikiwemo za
daraja la tatu ambazo zimenipa mwaliko, lengo ni kujifunza na kama nikipata
nafasi kidogo nitakwenda Uswiss katika klabu ya Basel ambako ni mwendo wa
dakika 25 kutokea hapa nilipo sasa, panaitwa Freiburg.
Kidogo baridi ni kali, lakini kiana
mapambano yanaendelea na tutakuwa tukiendelea kujuzana na mambo mengine hasa
makala, natupia kwenye CHAMPIONI pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment