June 26, 2013



 
Mwisho wa maisha ya mshambuliaji Carlos Tevez nchini England umefika baada ya klabu yake ya Manchester City kukubali kuchukua kitita cha pauni milioni 10 kutoka kwa Juventus.

Mabingwa hao wa Italia wameonyesha nia yao ya kumchukua Tevez tokea miezi mitatu iliyopita na Jumanne ijayo kila kitu kitafikia mwafaka.



Tevez, 29, atasaini mkataba wa miaka mitatu na Juve maarufu kama Vibibi Kizee vya Turun lakini kabla atapima afya yake Jumanne.

Imeelezwa jana ndiyo siku ambayo klabu hizo mbili zilifikia makubaliano baada ya Meneja Mkuu, Beppe Marotta na Mkurugenzi wa Michezo wa Juve, Fabio Paratici kwenda jinni Manchester na kumaliza suala hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic