Mabingwa watetezi mara mbili wa
michuano ya Kombe la Kagame, Yanga wametangaza kujiondoa kushiriki michuano
hiyo.
Kupitia mtandao wake, Yanga
imethibitisha kujitoa katika michuano hiyo ambayo kama wangeshinda wangekuwa
wamebeba kombe mara ya tatu mfululizo.
Maana yake baada ya kushinda kombe hilo
mara mbili mfululizo, Yanga imeamua kujivua ubingwa.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika
nchini Sudan na Yanga imechukua uamuzi huo kutokana na vigezo vya hofu ya
kutokuwa na amani ya kutosha nchini humo.
Hofu kubwa ilikuwa ni katika jimbo la
Darfur ambalo limekuwa na mapambano ya silaha mara kwa mara.
Kutokana na uamuzi huo, tayari Baraza
la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limeialika URA ya Uganda
kuchukua nafasi hiyo ya Yanga.
Bado URA haijaeleza kama itachukua
nafasi hiyo, lakini Shirikisho la Soka Uganda (Fufa) limekiri kupotea barua
hiyo.
Timu nyingine ya Tanzania itakayoshiriki
michuano hiyo ni Simba nab ado haijajulikana itachukua uamuzi gani kuhusiana na
hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment