Kiungo Humud Abdulhalim ametua kimyakimya na kujiunga na kambi ya Simba iliyoko Bamba Beach, Kigamboni jijini Dar.
Humud aliyekuwa Azam FC na baadaye ikaelezwa kuwa ameshajiunga na timu ya daraja la kwanza nchini Afrika Kusini, sasa amerejea Simba.
Hata hivyo imeelezwa atakuwa akiendelea na mazoezi na Simba nab ado hajajihakikishia usajili hadi atakapojadiliwa.
Pamoja naye, beki Vincent Mabusela kutoka Black Leopard ya Afrika Kusini naye alikuwa akiendelea na mazoezi na kikosi hicho chini ya Abdallah Kibadeni.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment