July 15, 2013



 
Kiungo nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham amemshauri mshambuliaji Wayne Rooney kuendelea kubaki OT.

Rooney amekuwa hana raha tena katika klabu hiyo na ameshaandika barua kuomba kuondoka lakini uongozi wa Man United pamoja na Kocha David Moyes wametaka mshambuliaji huyo abaki.
BECKHAM (KUSHOTO) AKIWA NA WAKONGWE WA ENZI ZAKE WAKIWA MAN UNITED AMBAO NI SCHOLES, BUTT, GIGGS, PHILL NA GARRY NEVILE

Wameishatangaza kwamba Rooney hatauzwa pamoja na juhudi za Chelsea na Arsenal kuonyesha wanamhitaji.

“Kwa kuwa Rooney ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu, naona sehemu anayostahili ni Manchester, hivyo itakuwa vizuri kama atakubali kubaki,” alisema.

Dalili zinaonyesha Rooney ataendelea kubaki United lakini Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amekuwa akiendelea kumshawishi kwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari kwamba anahitaji ajiunge naye Stamford Bridge.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic