July 3, 2013



 
Kipa mpya wa Yanga, Deogratius Munishi 'Dida' ameanza mazoezi rasmi chini ya kikosi cha Mholanzi, Ernie Brandts.

Dida ameungana na wachezaji wengine wa Yanga kwenye Uwanja wa Loyola, Mabibo jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi chini ya Mholanzi huyo.



Dida ambaye aliwahi kuwa kocha wa Simba amejiunga na Yanga ka mchezaji huru baada ya mkataba wake na Azam FC kwisha.
Sasa kipa huyo atakuwa namba mbili kwa kuwa Ally Mustapha ‘Barthez’ tayari ndiye kipa namba moja wa Yanga kwa sasa.

Pamoja na Dida, wengine walioanza mazoezi ni Shaban Kondo aliyekua akicheza soka nchini Msumbiji pamoja na beki wa kati, Rajab Zahir aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akifanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.


Wachezaji wengine wa Yanga ambao walianza mazoezi jana akiwemo Mrisho Ngassa wamejiunga na kikosi cha tikmu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa kuivaa Uganda katika michuanonya Chan.

Hadi sasa, tayari Yanga imesajili wachezaji wapya watano ambao Dida (huru), Rajab Zahir - Huru (Mtibwa), Mrisho Ngassa - Huru (Azam), Shaban Kondo  -  Huru na Realitus Lusajo - Machava FC.

Kocha wa Yanga, Brandts alirejea nchini juzi na kuanza kazi jana na amesisitiza wachezaji wake kujituma kwa ajili ya kujenga kikosi imara zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic