July 18, 2013




Kocha Mkuu wa Liverpool, Brendan Rodger amewapa wachezaji wake mazoezi makali bila ya kujali hali ya hewa mbaya.

Ingawa hali ya hewa nzito ya joto lla uvuguvugu nchini Indonesia, lakini Rodgers alisisitiza lazima wafanye mazoezi makali.


Pamoja na wachezaji kuonyesha kuwa hali ilikuwa ngumu kwao, lakini Kocha huyo alisisitiza suala la kuendelea na mazoezi.

Katika mazoezi hayo alifundisha namna ya kucheza na timu mbalimbali kutegemeana na uchezaji wa timu pinzani.

Baadaye aligawa vikosi viwili na gozi likaanza kusukumwa kwa kasi utafikiri mechi ya ukweliukweli.
Liverpool iko nchini Indonesia ikiwa ni moja ya nchi ambazo inafanya ziara barani Asia.



TIMU YA KWANZA:  Mignolet, Enrique, Skrtel, Kelly, Agger, Downing, Coutinho, Lucas, Alberto, Gerrard, Aspas
TIMU YA PILI: Jones, Flanagan, Wisdom, Toure, Johnson, Sterling, Allen, Borini, Henderson, Assaidi, Ibe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic