Manchester
United imeamua kukata mzizi wa fitina na sasa imeweka mezani pauni milioni 26
ili kumsajili kingo wa Barcelona, Cesc Fabregas.
Uamuzi
huo wa United umetokana na timu hiyo kumkosa kiungo mshambuliaji mwingine
Thiago Alcantara ambaye amesajiliwa na Bayern Munich.
Kocha
David Moyes anataka kumuunganisha Fabregas kwa mara nyingine na Robin van
Persie.
Wawili
hao walicheza kwa ushirikiano mkubwa wakati wakiwa katika kikosi cha Arsenal na
Fabregas ,26, alimuachia van Persie utepe wa unahodha.









0 COMMENTS:
Post a Comment