Kocha Mkuu wa
Yanga, Ernie Brandts amelalama kuwa viwanja vya mikoani kuwa ni hatari kwa
wachezaji.Akizungumza jijini Dar, Brandts alisema viwanja vingi vya mikoani ni hatari wa wachezaji kwa kuwa viko katika hali mbaya sana.
“Ni hatari na si kitu kizuri kwa wachezaji kwa kuwa viko katika mazingira mabaya sana.
“Mfano uwanja wa Tabora hakuna majani hata kidogo uwanjani, ni vumbi tu na nimeambiwa utatumika katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Hii si sahihi, hili suala liangaliwe.
“Ninashauri ikiwezekana viwanja vikaguliwe kabla ya kuruhusiwa kutumika ili kuwalinda wachezaji na pia kuipa hadhi ligi hii. TFF waliangalie hili,” alisema Brandts.
Yanga ilifanya ziara katika mkoa wa Tabora, Mwanza na Shinyanga na kucheza mchi za kirafiki lakini haikuonyesha kama ni tishio.







0 COMMENTS:
Post a Comment