July 11, 2013


OLOYA AKIWA KAZINI NCHINI VIETNAM...


Mshambuliaji Moses Oloya wa Saigon ya Vietnam amewahakikishia Simba kwamba atatua katika klabu hiyo.

Oloya raia wa Uganda amewaambia Simba kuwa ameamua kujiunga na timu hiyo bila ya kujali amekuwa akipata ofa kutoka katika timu mbalimbali za Tanzania na kwingineko.


“Oloya amekuwa akitakwa na timu nyingi, ziko za Tanzania nay eye anaonyesha amepania kurudi Afrika. Hivyo amezungumza na Simba na kuwaeleza kila anachotaka.


“Tayari wamekubaliana na amekuwa akifanya mazungumzo na klabu yake ikiwezekana imuachie mapema yaani mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kwisha ili akiondoka Vietnam asirudi.

“Simba wamekubali kumlipa mshahara wa mwezi mmoja ambao atakuwa amevunja kule. Inawezekana na Wavietnam hao pia wanaweza kukubali kwa kuwa baada ya ligi kwisha atakuwa amebakiza mkataba wa mwezi mmoja,”kilieleza chanzo cha uhakika.

Yanga pia imekuwa ikimuwania mchezaji huyo kutokana na ombi la kocha wao, Ernie Brandts lakini viongozi wake wamekuwa wakijaribu kutaka kuficha kwa kuhofia kuonekana wanamfuatilia.

Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kumfuata, Yanga wakafuatia na kusababisha mshambuliaji huyo mwenye kasi kuwa gumzo kubwa nchini.
Bado haijajulikana katika vita hiyo nani ataibuka mshindi na kumpata mchezaji huyo kwa ajili ya msimu ujao.

1 COMMENTS:

  1. Salehe Ally namuomba sana Mwenyezi Mungu aendelee kukupa nguvu na pumzi ili uendelee kutuletea habari nzuri na za uhakika kama hizi...MSAFIRI KAGEMA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic