July 4, 2013



 
Beki wa zamani wa Manchester United, Phil Neville amerejea katika klabu yake hiyo ya zamani.

Nevile amependekezwa kuwa kocha wa timu ya kwanza, timu ambayo inafuatia baada ya ile timu kubwa ya Manchester United.


Leo asubuhi, Neville ambaye kaka yake Gary amecheza hadi kustaafu akiwa na Man United, aliwasili katika makao makuu ya kabu hiyo eneo la Carrington.

Kocha mpya wa man United, David Moyes amempendekeza Neville kuchukua nafasi hiyo kwa kuwa walifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa wakati yeye akiwa kocha we Everton na beki huyo akiwa nahodha wa kikosi chake.

Mwezi uliopita, Neville,36, alitangaza kustaafu kucheza soka na kuhitimisha miaka yake 18 ya kucheza soka la kulipwa. Ndugu yake Garry ni kati ya memba wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic