July 4, 2013



VAN GINKEL (KUSHOTO) AKIPAMBANA

Kocha Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho ameendelea na usajili wake kwa kumsainisha kiungo kinda wa Vitesse Arnhem, Marco van Ginkel.

Mourinho ameanza usajili na mshambuliaji Schurrle kutoka Bayer Leverkusen, sasa amemchukua kinda huyo kwa kitita cha pauni milioni 9.


Van Ginkel,20, raia wa Uholanzi na mmoja wa wachezaji makinda wa timu ya taifa ya nchi hiyo ameonyesha kumvutia zaidi Mreno huyo.

Mwaka 1999, Van Ginkel alijiunga na Vitesse akiwa na umri wa miaka saba. Aliendelea kufanya vizuri hadi alipopata kwa mara ya kwanza nafasi katika kikosi cha kwana, hiyo ilikuwa mwaka 2010.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic