Baada ya kufungwa na Morocco na Ivory
Coast kwenye michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia
mwakani, Tanzania imeporomoka kwa nafasi 12 kwenye ubora wa soka dunia.
Katika msimamo uliotolewa na
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) jana, Tanzania imetupwa hadi nafasi ya
121 kutoka nafasi ya 109 iliyokuwa mwezi uliopita.
Hali hii imetokea kutokana na matokeo
mabaya ya michezo hiyo miwili ya mwezi uliopita, awali ilichapwa na Morocco
mabao 2-1 na ikaja nyumbani ikakubali kichapo cha mabao 4-2 toka kwa Ivory
Coast.
Hispania imeendelea kuongoza kwa
ubora duniani ikiwa katika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Ujerumani, huku
nafasi ya tatu ikishikwa na Colombia.
Ivory Coast wanashika nafasi ya 13
kwa ubora duniani wakiwa nafasi ya kwanza kwa ubora Afrika. Tanzania inashika
nafasi ya 35 kwa ubora huo kwa bara la Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment