Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie
Brandts ameonyesha kukerwa na kitendo cha wachezaji wake wawili kushindwa
kutokea katika mazoezi leo.
Yanga ilianza mazoezi leo
asubuhi na wachezaji watatu tu hawakutokea ambao Haruna Niyonzima, Kelvin
Yondani na Athumani Idd ‘Chuji’.
Akizungumza na Salehjembe,
Brandts raia wa Uholanzi alisema hakufurahishwa na kitendo cha Yondani na Chuji
kutotokea mazoezini.
“Meneja aliniambia wote
aliwasiliana kasoro Niyonzima pekee ambaye hakufanikiwa kumpata. Lakini Yondani
na Chuji hawajaja mazoezini.
“Wao ni wachezaji wa timu ya
taifa pia, walipaswa kuwa mfano na kujua nini cha kufanya, sijafurahishwa na
kitendo hicho na ninatapenda kupata maelezo watakapoanza mazoezi.
“Ila kwa sasa nimewapa
ruhusa wachezaji wote wa timu ya taifa kwa kuwa wataanza mazoezi kesho, najua
pia wao wataungana na timu ya taifa lakini nitazungumza nao wakirudi,” alisema
Brandts.
0 COMMENTS:
Post a Comment