Pamoja na kukubali sasa kwamba iko tayari kutoa euro milioni 35 kumtwaa beki wa Chelsea, David Luiz, Barcelona imeonyesha kuanzisha uchokozi wa wazi.
Carlo Ancelotti ametamba kikosi chake cha Real Madrid kitakuwa na aina mpya ya uchezaji ambayo itakifanya kuwa bora kuliko vingine.
Ancelotti amesema amekuwa akifanya kila linalowezekana kuwa na aina ya kipekee cha uchezaji na sasa imepatikana.
“Nitatumia fomesheni ya mti wa mkrismass ambayo ni 4-3-2-1, hii ni bora kwa kuwa kutakuwa na viungo watatu na washambuliaji wawili wanaomsaidia mmoja aliye juu,” alisema.
Katika mechi za kirafiki kujiandaa, Ancelotti alitumia mifumo mbalimbali na ule wa 4-4-2 aliutumia sana.
Mifumo yote miwili pia ilikuwa inatumia na kocha wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho hata hivyo kuna tofauti wakati timu hizo zinashambulia.
Ancelotti tayari amesema kikosi alichonacho sasa chini ya kocha msaidizi Zinedine Zidane ni bora zaidi kuliko alichowahi kuwa nacho awali.








0 COMMENTS:
Post a Comment