MENEJA WA CASTLE, KABULA NSHIMO AKIWA NA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, FENALLA MUKANGARA |
$$$$$
CASTLE LAGER YAANZA
KUIDHAMINI FC BARCELONA
MASWALI NA MAJIBU KWA
MKURUGENZI WA MASOKO WA TBL, BI. KUSHILLA THOMAS
1. Je Ushirikiano huu
unahusu nini?
Ushirikiano huu unaifanya, Castle Lager kuwa Bia rasmi Ya Afrika
inayodhamini FC Barcelona. Castle
ni bia bingwa ya Afrika ambayo inajitahidi kusimamia na kuendeleza
ukamilifu/ubora wake wakati FC Barcelona ni timu bingwa ambayo daima inalenga
kufikia mafanikio zaidi. Huu ni ushirikiano imara na ni matokeo ya mapenzi yetu
kwenye soka
2. Unajisikiaje kuhusiana na ushirikiano huu?
Nina msisimko mkubwa kuhusiana na ushirikiano huu na FC Barcelona
na Nina furaha kusema kwamba ushirikiano huu utaimarisha uhusiano kati ya
Castle Lager na wateja wake wa Afrika ambao ni mashabiki wazuri wa timu hii
ambayo inaangaliwa na kufuatiliwa na wapenzi wa soka duniani kote.
3.
Castle itafaidika vipi na ushirikiano huu?
Kupitia ushirikiano huu, Castle Lager itakuwa ni bia pekee Afrika yenye
haki za kipekee kutumia Nembo ya FC Barcelona, rangi, na picha za
wachezaji katika mawasiliano ya bidhaa ya Castle kama vile matangazo ya aina
zote nk. Tunaamini kwamba ushirikiano huu Utajenga uhusiano kati ya FC
Barcelona na watumiaji wa bia ya Castle Lager. Aidha kutakuwa na shughuli
mbalimbali zinazohusu kuendeleza mpira Tanzania zikiendelea na maeneo
mengine ya Afrika inakopatikana bia ya Castle.
Bia ya Castle inatambuliwa kama mdhamini Mkuu wa mpira wa miguu na
matukio mengine mengi ya michezo Afrika na kimataifa. Ushirikiano huu kati ya
Barca / Castle ni kilele cha mafanikio ya udhamini wa michezo.
4.
Ina maana gani kwa mashabiki wa soka na watumiaji/wateja wa CASTLE katika
Nchi yako?
Tunataka kuhakikisha kwamba tunaimarisha undugu huu katika soka la
Tanzania na hasa mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya ushirikiano huu
wa kusisimua. Maelezo zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini
Dar es Salaam tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki
katika mfululizo wa shughuli za soka za kikanda / kanda ambazo ni za
kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii, kuwazawadia mashabiki wetu
waaminifu wa Castle/Barca. Kupitia ushirikiano huu Castle Lager
itahakikisha kila shabiki anafurahia wakati kamili
5.
Je Ushirikiano huo utakuwa na manufaa chanya
kwenye jamii Nchini kwako?.
Hakika, Mashabiki wa Barcelona Tanzania na jamii zao kuna mengi ya
kusuburia, Castle Lager ina mipango mikubwa ya kuifikia jamii kwa maendeleo
kwenye mikoa zaidi ya nane nchini.
Tunataka kuhakikisha kwamba
tunaimarisha undugu huu katika soka la Tanzania na hasa
mashabiki wa FC Barcelona ambao ni sehemu ya
ushirikiano huu wa kusisimua. Maelezo
zaidi yatafafanuliwa wakati wa uzinduzi wa kitaifa jijini Dar es Salaam
tarehe 17 Agosti na wapenzi wa soka wa Tanzania watashiriki katika mfululizo wa
shughuli za soka za kikanda / kanda
ambazo ni za kuhamasisha. Kutakuwa na shughuli za kijamii kuwazawadia mashabiki
wetu waaminifu wa Castle/Barca. Kupitia ushirikiano huu Castle Lager
itahakikisha kila shabiki anafurahia.
0 COMMENTS:
Post a Comment