August 26, 2020


 BAADA ya uongozi wa Yanga kusema kuwa unashangazwa na shinikizo kutoka kwa Wizara ya Uhamiaji kuitaka timu hiyo kutoa kibali cha kazi kwa nyota wao wa zamani, Bernard Morrison, Simba nao wamewajibu kimtindo watani zao wa jadi.

Morrison alikuwa kwenye mvutano mkubwa na mabosi zake Yanga kwenye ishu ya mkataba ambapo yeye alikuwa anadai kwamba ana dili la mwaka mmoja huku Yanga wakieleza kuwa ana dili la miaka miwili.

Shauri hilo lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10 mpaka Agosti 12 ambapo majibu yalipotolewa makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) yalieleza kuwa Morrison ni mchezaji huru na ameshinda kesi yake hiyo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa:"Naishangaa Wizara ya Uhamiaji inaposhinikiza tutoe kibali cha Morrison, inaonesha kama kuna 'Interest'. Kama kutolewa kinatolewa lakini kwa taratibu maalumu."

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amejibu namna hii:"Nimeskia mmoja kaanza kuilaumu Wizara ya Uhamiaji , sikujua kuwa Bongo kuna hii wizara."

21 COMMENTS:

  1. Watafanya nini Yanga kutokana na kukataa amri ya uhamiaji halali ya kutaka kukirejesha kibali cha kazi cha Morrison pindi uhamiaji nayo ikaamuwa kutokutoa vibali vya kazi vya wachezaji wao wwa nje?

    ReplyDelete
  2. Utopolo wanatapatapa, kibali watatoa tu watakewasitake, washazoea kitonga Cha enzi ya malinzi

    ReplyDelete
  3. Mkataba WA swali WA Morrison Ni mwaka au miezi sita?

    ReplyDelete
  4. Anaetoa kibali ni uhamiaji, wanaweza kukifuta tuu na kutoa kipya, ubishi wa nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ili uombe na upewe kingine lazima yule aliyekuombea kibali cha awali aandike barua ya kutokuwa na pingamizi lolote kwa wewe kupewa kibali kipya hivyo lazime yanga watoe ruhusa ya Morrison kupewa kingine

      Delete
  5. Kama wanatoa vinali kwa nn wakifuate kilichopo yanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utaratibu uko hivyo lazima mwajili wa zamani aulizwe kama anapingamizi lolote kwa mtu wake kupata kibali kipya akiwa amehamia kwa mwajili tofauti

      Delete
  6. Ihamiaji wanaanzaje kukataa kukataa kutoa kibali.sheria IPO wazi lazima watoe. Swala la kibari halina usimba na uyanga ishu ya Morrison uhamiaji wasubiri rufaa ya yanga CAS











    ReplyDelete
    Replies
    1. Idara ya Uhamiaji inamuhusu nini na rufaa ya Yanga huko CAS? FIFA/CAS ndio anahusika na vibali vya kazi vya nchi husika? Aliyetoa hukumu ni TFF kuwa mchezaji huyo yuko HURU na anaweza kwenda kuchezea timu anayotaka.Hivyo hukumu hiyo ya TFF bado ina exist na haijatenguliwa na sijui ni kifungu gani cha sheria kinachosema mchezaji akiwa ana kesi au amekatiwa rufaa hawezi kuajiriwa au kusajiliwa? Vipi hiyo rufaa ikisikilizwa mwakani?Itakuwa fair kwa mchezaji kukaa bila kuajiriwa/kucheza eti sababu anasubiria rufaani aliyokatiwa?

      Delete
    2. Mfumo mpya hauruhusu mchezaji kusajiliwa kwa vikaratasi kama zamani.FIFA ndiyo yenye mfumo wa TMS.Simba wakishindwa kuingiza jina lake kwa kuwa tayari lipo kwenye mfumo wataishitaki yanga kwa kuwa na jina la mchezaji wao, hapo ndipo Fifa wataiuliza Yanga kwamba kwa mini umemweka mchezaji huyo kwenye mfumo na yanga itasema nina mkataba naye huyo mchezaji na mkataba huu hapa.Hakuna uwezekano wowote ukute mchezaji anasoma timu mbili kwenye mfumo wa TMS.Yule aliye mwingiza kwenye mfumo na ameweka mkataba wa huyo mchezaji ndiye mmiliki halali wa mchezaji.Haspop na Magori wako kizamani wanafikiri inawezekana kutumia kamati za TFF kupata mchezaji kumbe hamna.

      Delete
    3. Kwani nani amekwambia kuwa Magori na Hanspope ni wanasheria kitaaluma? Kwa akili yako unafikiri Simba haina wanasheria?

      Delete
  7. yanga ipo juu ya serekali? hahahahahhaa

    ReplyDelete
  8. Wasubiri rufaa ya yanga, iko wapi iyo rufaa? C ndo kawaida yao kusema uongo? Kibali watatoa

    ReplyDelete
  9. Kama hahawatatoa na wao hawatopewa nawachaguwe watakalo

    ReplyDelete
  10. Morrison tayari yuko kwenye mfumo wa FIFA na anatambulika mchezaji wa Yanga na hakuna namna unaweza kuingiza jina LA mchezaji yuleyule tena lazima yanga imuondoe kwenye mfumo.Anaye weza kuilazimisha na kuiamuru yanga imfute Morrison kwenye TMS ni FIFA pekee yake.Hivyo Simba hawataweza kumuingiza tena labda wabadirishe jina.Yanga ikisha ambiwa na FIFA imuondoe ndipo itamutoa.USAJILI wa kwenye makaratasi ulisha pitwa na muda hakuna ujanja tenaaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aliingizwaje kwenye mfumo wa TMS wakati dirisha la usajili lilifunguliwa 1st Aug?....hivi inaingiaje akilini kamati ya Sheria itoe hukumu kuwa mchezaji yuko huru huku aikaange TFF yake akijua ameshasajiliwa kwenye TMS?kama itakuwa hivyo basi na TFF yuko kikaangoni

      Delete
    2. Tatizo TFF ni tawi dogo la simba ndiyo maana simba wamejaa viburi kwamba kila kitu kwao ni rahisi hebu tusubiri matokeo halafu tukutane kwa hoja humu ila tusikimbiane

      Delete
    3. vile vile TFFni tawi kubwa laYanga mpira mmeshindwa mmebaki kushindana kuimba taarabu subirini mbungi ianze alafu tuone

      Delete
  11. Kama kinatolewa lakini kwa taratibu maalim. Kwa ufupi hapa ina mana Yanga intaka ilipwe hela

    ReplyDelete
  12. Habari mpya zinasema Yanga inadai ilipwe Shilingi milioni Mia sita ili iwe funzo kwa wengine tena wanasema kwakujiaminini. HAHAHAAAA. Tutaona vioja vingi mwaka huu, hasa pale vichapo vitapoanza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic