August 11, 2020



 MWENYEKITI wa Kamatiya Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF), Elias Mwanjala amesema kesi ya Bernard Morrison itaendelea kuskilizwa kesho.

Kiungo wa Yanga, Morrison alikuwa na mvutano mkubwa na klabu ya yake kuhusu sakata la mkataba ambapo yeye anadai kwamba ana dili la miezi sita ambalo limekwisha huku Yanga ikieleza kuwa ana dili la miaka miwili.

Sakata lake leo ni siku ya pili ambapo lilianza kusikilizwa jana, Agosti 10 na leo Agosti 11 pia limeskilizwa na hakuna majibu ambayo yametolewa.

Mwanjala amesema kuwa kuna document  moja haijakamilika kwa pande zote mbili ya Yanga na Morrison  na pande zote zimesema jioni ya leo watazileta.

"Kuna nyaraka ambazo hazijakamilika kwa pande zote mbili, moja ya Yanga na moja ya Morrison jambo ambalo limefanya tushindwe kutoa maamuzi.

"Kesho zitakabidhiwa kwa kamati ambapo kikao kitaanza kesho saa 4 asubuhi kufikia saa saba na nusu kesho kikao kitakuwa kimekwisha na watatoa maamuzi juu ya kesi hiyo."

Morrison Agosti 8 kesi yake ikiwa bado haijatolewa hukumu alitambulishwa na watani wa jadi Simba huku ikielezwa kuwa amesaini kandarasi ya miaka miwili jambo linaloongeza mvutano wa uhalali wake.

  

24 COMMENTS:

  1. Tff wanaboa na ndio wanaoharbu mpira. Kwa ajl ya uyanga na usimba

    ReplyDelete
  2. Mwenyekiti wa kamati sema ukweli. Forgery ni kosa la jinai.

    ReplyDelete
  3. Jamani aibu hii tukajifiche wapi!!

    ReplyDelete
  4. jaman hawa watu kesi ya kuangalia mkataba kama ni halali au sio halali inachukua siku 3?

    ReplyDelete
  5. Mwanjala na Uyanga wake....mahaba niue

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi hapa Uyanga na Usimba unatoka wapi hapa issue ni Simba kujiingiza ktk issue zisizo wa husu,Mimi nadhani 1Kuna watu wanajiita wa mpira wapimwe uadirifu wao,2 Tuwe wa kweli kwa nini kuvizia ,Mimi nilitegemea Timu inayoendeshwa kisasa Kama Simba isiwe chanzo cha choko choko ?na hizi media za watu wa Simba tuzipime pls , Magazeti yote ya michezo ,Fm Redio zejaa Simba na hao watu hata akiwa na cheo Cha jamii hawana nyongo tuliona mtu mmoja mpaka ana kaa benchi la ufundi

      Delete
    2. Kesi hii ni ya Utopolo na Morrison. Simba wanaingiaje hapo? Mchezaji amesema mmegushi mkataba.

      Delete
  6. Hakuna kitu hapo, ukweli uwekwe wazi waliona makosa waadhibiwe

    ReplyDelete
  7. Kwani wapenzi wa Simba hii issue hamjui Kama mmeharibu kwa kuvizia na kuchungulia ndoa za watu

    ReplyDelete
  8. kaa la Moto issue ya Morrison na yanga,na Simba na yanga ,TFF na vilabu vyake.hapa ndo busara za vio ngozi was TFF zinatakiwa na haki itendeke ili wachezaji na vilabu wakumbushwe uadilifu na MAWAZO ya kipuuzi kwa wadau wachache wa mpira wakome.rais karia umelifanyia soka la bongo TZ mengi mazuri,na hili ni mboga kwako maliza na utoe fundisho.zaidi watu waheshimiane.siyo fedha iheshimishe mtu.utu kwanza.asanteni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww unafikiri kinachokwamisha ni nn km sio kugundurika jamaa wamegushi Spain.

      Delete
    2. Hii ndio iwe Fair Decision: Morrison awe mchezaji huru.....Yanga mkataba uwe ulikwisha na mkataba waliousaini bado ulikuwa na mapungufu na kwa Simba uamuzi uwe hawakufuata utaratibu na walikiuka kanuni!

      Delete
  9. Hilo swala maamuz yake n magumu kwasababu hyo timu inaweza kushushwa daraja

    ReplyDelete
  10. Hii ndio iwe Fair Decision: Morrison awe mchezaji huru.....Yanga mkataba uwe ulikwisha na mkataba waliousaini bado ulikuwa na mapungufu na kwa Simba uamuzi uwe hawakufuata utaratibu na walikiuka kanuni!

    ReplyDelete
  11. Simba ndo wanaolindwa hapo,hv tff ni kweli hawajui mkataba wa Morison na Yanga?TFF acheni kuharibu mpira kama mmeshindwa bwageni manyanga

    ReplyDelete
  12. Utopolo wamefoji barua ya Abubakar Salum wa Azam kwamba aliandika barua ya kuomba kuondoka. Wamewasilisha barua imeandikwa tarehe ya kesho 12 Augusti 2020. Ilipelekwa na Yanga kwa Azam. Abubakar amekanusha kuandika barua hiyo.Azam wameitaka Yanga kuacha mchezo mchafu na waombe radhi. Wazee wa forgery.

    ReplyDelete
  13. Tatizo ni Elias Mwanjala ambaye ndio mwenyekiti wa kamati. Ni mwanachama wa Yanga ba alishindwa kwenye uchaguzi uliopita wa Yanga.

    ReplyDelete
  14. Mtu mwenyew anaye ng'ang'ania hata nidhamu hana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo mwanjala juzi kashindwa uchaguzi mbeya tena alikuwa mgombea pekee hivi kama yanga waliwasilisha mkataba tff na kamati ilishapeleka sahihi polisi kinachowafanya washindwe kutoa maamuzi ni nn

      Delete
  15. Hao kandambili aka GONGOWAZI wamefoji mkataba na sio mara ya kwanza ndio staili yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic