February 7, 2020


FT:Simba 0-1 JKT Tanzania
Uwanja wa Uhuru
Adam Adam dk 24

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na JKT Tanzania umekamilikwa kwa Simba kubanwa mbavu kwa kufungwa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi limefungwa na Adam Adam dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza ambalo limedumu mpaka mwisho wa kipindi.

Nyota wapya wa Simba, Luis na Shiza Kichuya wameanza leo kwa mara ya kwanza.

Mashabiki wamejitokeza kushuhudia ushindani uliopo kwani leo ni mechi ya kisasi.

Mchezo wa kwanza walipokutana Simba ilishinda mabao 3-1 na leo kisasi kimelipwa kwa  JKT kushinda bao 1-0.

23 COMMENTS:

  1. Wachezaji wazuri fest 11 wanaachwa nje huku kocha akili anayo sawa niliwahi kusema tunafukuza kocha mzuri tunachukuwa mpumbavu bora tufungwe 2 hakuna kocha ujinga mtupu huyo mchezaji wa msumbiji kichuya watu wamekula pesa wamesajiliwa wa nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usihofu sana kwani upo uwezekano mkubwa wa magoli ya offside kwenye dakika za lala salama

      Delete
  2. Hahahaha unataka utolewe
    povu la kujaza ndoo nzima@yanga damu

    ReplyDelete
  3. wanasimba msihofu mlienda naushindi mtashinda 2-1. off side zipo

    ReplyDelete
  4. uongozi wa simba walitazame hili swala kwa jicho jingine,simba inaenda kupoteza ubingwa msimu huu kama watamuacha kocha huyu afanye anavyotaka,naona kwa mtazamo wangu huyu kocha hana ushirikiano kabisa na benchi la ufundi anafanya kila kitu kama yy mwenyewe,simba imepoteza ladha ya mpira kabisa,wanacheza very slow kana kwamba wao tuu ndio wanachoka kuliko timu nyingine inayocheza mechi kila baada ya
    siku mbili,viongozi simamieni hili,simba kwasasa inatia mpaka aibu kwakweli.

    ReplyDelete
  5. Tulikuwa tunawaambia ushindi wenu wa magoli ya Off side mkaona kama hatuwatakii mema sasa leo marefa wameamua kuwabania magoli yenu ya kuotea, mnaona mnavyopata tabu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. siyo marefa waliowabania bali ni watanzania wameamua kuungana na kulipigia kelele swala la offside: serikali, wabunge, wachambuzi wa soka, waamuzi wastaafu, wachezaji wastaafu, waandishi wa habari, wasanii, wadau, makocha na wapenzi wamekuwa na nguvu ya kuyazuia magoli ya offside. Waendelee kumsikiliza Manara anayewaaminisha kuwa hata polisi hawawezi kufanya lolote

      Delete
  6. Salaa laa,duh,kapigwa leo,manara nenda polisi kashtaki wewe sasa

    ReplyDelete
  7. Kwa mpira huu ujinga huu na kocha huyu hata kombe la mbuzi hatuchukuwi tusahau kabisa nakushauri NO achana na hii timu mm ni mwanachama wa simba sio kwa simba hii umewekeza pesa nyingi sana sana upumbavu wa namna hii

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakushauri usikate tamaa kwani bado kuna offsides nyingi tu zitaokoa jahazi

      Delete
  8. Nyie mnataka kila mechi mshinde tu mkifungwa tatizo kocha,haya mleteni wenger

    ReplyDelete
  9. Baca anafungwa Spain sembuse Simba ya Tz?

    ReplyDelete
  10. Bebwabebwa fc Leo marefa offside hawakuziona au?mbona sielewi au Leo wamepewa jkt tz

    ReplyDelete
  11. YANGA jihadharini kesho watatumia nguvu ya pesa kuwarudishia wapenzi wao furaha. Watafanya kila njia mfungwe. Vyumbani ingieni na LITMUS PAPER. Wana vichupa vyao hao tangia enzi za CAF champions. Thibitini wachezaji wenu. Simba ilikuwa ile ya Okwi siyo.

    ReplyDelete
  12. Simba inatumia mbinu chafu sana kuwadhohofisha timu pinzani ikiwemo hiyo ya kupuliza madawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Una ushahidi? Mbona hata mechi za ugenini wanashinda.

      Delete
  13. Wawa bado ana udhaifu wa kufanya blocking anakaba kwa macho. Midfielders wana udhaifu wa kupiga mashuti nje ya box ndio maana ushindi ni wa taabu. Timu zote zinapaki basi hakuna namna nyingi zaidi ya kubadili game plan. Nafasi ya ubingwa kwa Simba ni kubwa sana kwasababu timu pinzani ni dhaifu mno.

    ReplyDelete
  14. Kawaida kwenye soccer timu ikishinda ya nashabiki ila ikifungwa ya kocha

    ReplyDelete
  15. Vyura mnachonga sana ila kuifikia Simba ilipo itawachukua mda sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic