Hatimaye Kampuni mpya ya Azam TV
imesaini mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuonyesha
Ligi Tanzania Bara.
Mkataba huo wa miaka mitatu utagharimu
Sh bilioni 5.6 na bodi hiyo italipwa kwa mafungu matatu, ikimaanisha kila
msimu.
Azam TV itakuwa na chaneli 50 na wiki
ijayo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wake, Rhy Torrington itaanza kurushwa
kwa majaribio kuanzia wiki ijayo.
Hata hivyo, Torrington amesema
hatakubali kuona Azam TV inaanza kuonekana kama hataridhika na kiwango chake
cha matangazo.
Kabla ya hapo, pande hizo mbili
ziliingia mkataba wa awali (MOU) na leo mkataba huo umesainiwa rasmi leo na
unaanza kufanya kazi mara moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment