Beki kiraka wa AS Cannes ya Ufaransa, Shomari
Kapombe, hatarejea nchini kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars kutokana na
kufanyiwa upasuaji wa kidole cha mguu.
Kutokana na tatizo hilo, Kapombe atakuwa
nje ya uwanja kwa siku 15 na tayari Kocha Mkuu, Kim Poulsen ametangaza
kumuondoa katika kikosi chake.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Poulsen
amesema kutokana na majeraha hayo amemuondoa kiraka huyo kwenye kikosi chake
kitakachoivaa Gambia Septemba 8, ikiwa ni mechi ya kukamilisha ratibna tu.
“Nimemuondoa
Kapombe kwenye kikosi changu kitakachoivaa Gambia kutokana na kuuguza kidonda
alichofanyiwa upasuaji mguuni mwake.
“Kwa mujibu wa taarifa nilizopewa kutoka
huko (Ufaransa), Kapombe anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili sawa na
siku 15 akiuguza majeraha hayo kabla ya kuanza mazoezi mepesi.
“Alifanyiwa operesheni hiyo kutokana na
wadudu kuathiri sehemu ya kidonda aliyoumia akiwa huko, kidonda hicho
kimesababishia ashindwe kucheza baadhi ya mechi akiwa huko,” alisema Kim.
Kapombe amejiunga na AS Cannes baada ya
Poulsen kumruhusu aende kufanya majaribio ingawa Taifa Stars ilikuwa kambini
kujiandaa kucheza na Uganda.
Hata hivyo, kocha huyo hajaeleza kama
ameshamuongoza beki mwingine kuchukua nafasi yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment