August 13, 2013



 Barcelona huenda ikaanza Ligi Kuu Hispania bila ya wachezajiw ake wawili Cesc Fabregas na Pedro.

Fabregas na Pedro wote ni majeruhi na huenda wakaikosa mechi hiyo ya kwanza dhidi ya Levante, Jumamosi.

Kocha Tata Martino aliongoza mazoezi ya leo bila ya Fabregas na Pedro hali iliyoonyesha wanaweza kukosa mechi hiyo.

Febregas amekuwa akihusishwa na kuhamia Man United lakini inaonekana Barcelona haina mpango huo.

 
Hata hivyo hata kama watakosekana Fabregas na Pedro  bado kikosi cha Barca kinaweza kuwa fiti kuiangamiza Levante.

Barcelona ndiyo mabingwa watetezi na wana kazi kubwa ya kupambana na kulitwaa tena kombe kwa mara nyingine mbele ya washindani wao wakubwa Real Madrid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic