Mshambuliaji
wa Napoli ya Italia, Gonzalo Higuaín ya boti na kulazimika kushonwa nyuzi kumi
tu baada ya kufikishwa hospitali.
Taarifa kutoka
ndani ya klabu hiyo na kuripotiwa na gazeti moja la Italia zimeeleza, Higuain
raia wa Argentina aliumia wakati akiendesha boti iliyogonga mwamba katika
kisiwa cha Capri, nchini Italia.
Capri ni
kisiwa ambacho watalii wengi hupenda kwenda kupumzika na Higuain alikuwa katika
mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na Seria A.
Imeelezwa aliteleza
na kuangukia kwenye mawe hali iliyomsababishia majeruhi hayo na baada ya
kufikishwa hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Daktari katika Hospitali ya Capilupi, Mauro Ingrosso
amethibitisha kuumia kwa Higuain na kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
“Ni kweli na
tumemshona nyuzi kumi, kati ya hizo nane ni upande wa shavu na mbili chini ya
kidevu lakini anaendelea vizuri sana,” alisema.
Higuain
amejiunga na timu hiyo ya Italia akitokea Real Madrid ya Hispania na huu ni
msimu wake wa kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment