August 26, 2013



Katika kipindi cha kwanza, Chelsea ilitumia muda mwingi zaidi kujilinda huku Man United ikishambulia.
Pamoja na kufanya mashambulizi mengi, bado Man United pia hawakuwa makini kutumbukiza mipira wavuni.


Wakiwa nyumbani Manchester United wameshindwa kuwaangusha Chelsea baada ya sare ya bila kufungana.
Mechi hiyo haikuwa ya kusisimua sana ingawa Man United walifanikiwa kutawala mchezo hasa katika kipindi cha kwanza na Chelsea ya Jose Mourinho ikionyesha kujilinda zaidi.
Kwa sare hiyo maana yake Chelsea inaendelea kubaki kileleni kwa kuwana pointi saba baada ya kucheza mechi tatu.
Wayne Rooney alikuwa akishangiliwa mara kwa mara kutoka na uchezaji wake wa kutoa pasi za uhakika.
Hata hivyo, Man United ilionekana kutocheza kwa kushambulia kwa kasi kama ile iliyokuwa chini ya Kocha Alex Ferguson.

Kivutio kingine makocha wa Man City na Everton walikuwa Old Trafford kuishuhudia mechi ambayo hata hivyo haikuwa ya kuvutia sana kama ilivyotarajiwa.


Man Utd: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia (Young 67), Cleverley, Carrick, Welbeck (Giggs 78), Rooney, Van Persie.
Subs: Anderson, Smalling, Lindegaard, Kagawa, Buttner.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne (Torres 60), Oscar, Hazard (Azpilicueta 90+3), Schurrle (Mikel 87).
Subs: Essien, Lukaku, Schwarzer, Mata.

Booked: De Bruyne, Torres.
Referee: Martin Atkinson (W Yorkshire

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic