Mchezaji wa Coastal Union, Juma Hamad amepata majeraha katika sehemu tofauti za mwili baada
ya kushambuliwa na mashabiki wanaodaiwa wa Yanga, juzi katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo lilitokea muda mchache baada ya mechi yao dhidi ya Yanga kumalizika
wakijiandaa kutoka uwanjani hapo kwa ajili ya kwenda hotelini.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa Coastal, Mohammed Bin Slum amesema Juma amaumia baada ya kukatwa
na vioo vya basi lao ambalo lilishambuliwa na mashabiki wa Yanga.
“Wametushambulia
na wamesema wazi wanalipa kisasi kwa kwa kuwa msimu uliopita Yanga
walishambuliwa pale Kabuku. Wanapaswa kuelewa mashabiki wetu wako Tanga mjini
wala si Kabuku.
“Lakini
ajabu zaidi, Yanga walishambuliwa walipokuja Tanga na kutunga 2-0, sisi tukaja
Dar na kucheza nao, tukatoka sare ya bao 1-1. Sasa mbona hawakutushambulia kama
kweli ni kulipa kisa.
“Inaonyesha
wazi hawakuridhika na matokeo, ile penalti imewauma ndiyo maana wamefanya vile.
Hakika si kitu kizuri ingawa tunashukuru mchezaji anaendelea vizuri,” alisema
Bin Slum.
Upande wa
Kocha Mkuu wa Coastal, Hemed Morocco amelaani kitendo hicho na kusema hakikuwa
cha kiungwana na Yanga wanapaswa kukubali matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment