Kiungo mshambuliaji wa Coastal Union,
Haruna Moshi ‘Boban’ ameonyesha kiasi gani ameamua kubadili kwa kushangazwa na
mechi yao dhidi ya Yanga ilivyotawaliwa na ubabe.
Boban ambaye amejiunga na timu hiyo
akitokea Simba amesema hatutegemea kuona mechi hiyo ikitawaliwa na ugomzi namna
hiyo.
“Kwa kweli inasikitisha kuona uwanja
wa mpira unakuwa uwanja wa chuki na ugomvi, mimi nilichokuwa na kiwaza juu ya
mechi hiyo ni ushinda.
“Timu zote zina wachezaji wazuri,
hivyo nilitegemea mpira wa kikubwa, lakini matokeo yake ungomvi umetawala,
jambo ambalo siyo zuri,” alisema Boban.
Mara nyingi kila lilipotokea tafrani
katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 1-1, Boban alikuwa akijitenga mbali
na wachezaji wengine.
Huenda aliamua kufanya hivyo ili
kuepuka kuingia katika jazba ambazo zingesababisha afanye kitu kisichotarajiwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment