Mshambuliaji mpya
wa Yanga, Mrisho Ngassa ameishuhudia timu yake ikibeba Ngao ya Jamii kwa
kuichapa Azam FC kwa bao 1-0 akiwa jukwaani.
Ngassa
alikuwa katika jukwaa la upande wa mashabiki wa Yanga akishuhudia mechi hiyo
hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Mashabiki wa
Yanga waliripuka kwa furaha kubwa baada ya kumuona Ngassa akipanda jukwaani
hapo na kuketi.
Mshambuliaji
huyo anatumikia adhabu ya TFF kukosa mechi sita za mashindano hiyo ya Ngao ya
Jamii ikiwa ya kwanza.
Pia ametakiwa
kulipwa Sh milioni 45 kwa kuwa alichukua Sh milioni 30 za Simba na Sh milioni
15 ni nyongeza ya asilimia 50 kama adhabu.
Ngassa
alisaini kuichezea Simba lakini baadaye akasaini kuichezea Yanga hali iliyozua
mkanganyiko huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment