Semina kwa
ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I)
wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa 2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka
huu) katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza.
Mafunzo hayo
yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi Leslie Liunda,
Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam wakati kituo cha Mwanza
kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.
Kwa Dar es
Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba.
Kituo cha
Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi,
Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Kituo cha
Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Dar es
Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe,
Pwani, Ruvuma na Tanga.
Washiriki
wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si
vinginevyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment