Yanga imefanikiwa kuifunga Sport Club Villa ya Uganda mabao 4-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi nyingine ya kirafiki jana SC Villa ililala kwa idadi kama hiyo ya mabao kutoka kwa watani Simba, hivyo Yanga inakuwa kama imejibu mapigo.
Mabao ya Yanga yalifungwa Mrisho Ngassa katika dakika ya saba, kabla ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kufunga bao dakika 20 baadaye.
Dakika ya 30, Didier Kavumbagu alifunga bao la tatu na kufanya hadi mapumziko matokeo yawe 3-1 kwa kuwa Villa walipata bao katika dakika ya 18 mfungaji akiwa Moses Ndaula.
Mnyarwanda Haruna
Niyonzima alihitimisha karamu ya mabao baada ya kufunga la nne katika dakika ya
62.
Yanga ambayo ilikuwa
ikibadilibadili wachezaji wake katika mchezo huo ikiwa ni sehemu ya kujinoa na
msimu mpya wa 2013/2014 ilipata mabao yake kupitia kwa Mrisho Ngassa, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.Kipigo hicho kinafanana na kile ambacho Villa ilikipata katika mechi ya jana kutoka kwa Simba kwenye uwanja huo ambapo kulikuwa na maadhimisho ya Tamasha la Simba Day.
Kikosi cha Yanga kilianza hivi: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul , 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Mrisho Ngassa, 8.Salum Telela, 9.Didier Kavumbagu, 10.Jerson Tegete na 11.Haruna Niyonzima.







0 COMMENTS:
Post a Comment