*Timu mbili, moja ya ligi kuu zatoa macho, wakala wake alonga LIVE na Salehjembe
Na Saleh Ally, Strasbourg, UFARANSA
Beki nyota wa Simba, Shomari Kapombe ameonyesha kweli ana kipaji baada
ya kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Kapombe mwenye umri wa miaka 21 amefuzu kucheza soka katika timu mbili
moja ikiwa inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa.
Championi ambalo linaendelea kuranda nchini Ufaransa limepata taarifa
hizo za uhakika mjini hapa, lakini wakala wake Denis Kadito ameendelea kusisitiza kuomba timu hizo
ziwe siri hadi hapo atakapozungumza na Simba.
“Kweli Kapombe amefanya vizuri sana, tulimpeleka majaribio AS Cannes. Hii timu iko
daraja la nne, CFA, chini ya Ligue 1, Ligue 2 na National. Sababu ya kufanya
hivi ni kwamba timu za Ligue 1 zina 2nd team ambazo wanacheza
ligi hiyo ya 4 pamoja na AS Cannes.
“Kwahiyo basi, kwavile idea ilikuwa tumpeleke
highest division, inamaana akiweza kucheza AS Cannes, ataweza kucheza 2nd team
ya Ligue 1 club. Hapa tulikuwa tuna-avoid kumpeleka moja kwa moja Bordeaux
ambapo kulikuwa na uwezekano wa kumpeleka. Tukahofia kuunguza opportunity
incase level yake isingefikia. Tulichofanya, kupitia washirika wenzangu
Ufaransa, waliwasiliana na maScout wa Club mbalimbali za Ligue 1 kuja
kumwangalia katika mechi. Na timu huwa zinakuja kutafuta wachezaji AS Cannes.
“AS Cannes ni timu kubwa sema walifanya makosa
financially na management wakashuka kutoka Ligue 1 hadi hapo walipo. Hii ndio
timu iliyotoa kina Patrick Viera, Zinedine Zidane na Luis Fernandes (mchezaji
mkali wa 1980’s). Timu iko vizuri sana hata ukiongea na Kapombe atakueleza,”
alisema Kadito, wakala kijana aliyepania kuona Tanzania nayo inapata wachezaji
wa kulipwa barani Ulaya.
Taarifa zinaeleza tayari wakala huyo ameanza mazungumzo na Simba
kuhusiana na Kapombe kujiunga na moja ya timu hizo za Ufaransa. Hata hivyo,
umaarufu mdogo wa Tanzania katika soka huenda ukawa tatizo
Pamoja na kuwa mgeni katika soka la Ulaya, lakini Kapombe alionyesha
uwezo mkubwa na kuwashangaza baadhi ya mawakala wengine ambao walialikwa kwa
ajili ya kumuangalia.
Utulivu wake kwenye mpira, basi za uhakika na ujuzi wa kukaba,
zilionyesha kuwavutia mawakala wengi.
Suala la Tanzania kutokuwa maarufu kisoka, huenda ndiyo limekuwa hofu
kwao lakini tayari Kapombe amemaliza kazi yake, kilichobaki ni makubaliano tu
katika ya klabu itakayomtaka na Simba.
Salehjembe inaendelea kuranda anga hizi huku likifuatilia zaidi kujua
kuhusiana na mchezaji huyo kinda Mtanzania ambaye kama atapata nafasi, huenda
akawa amewasaidia Watanzania wengine kutoka.







0 COMMENTS:
Post a Comment