Siku 767 baada ya kurejea Arsenal,
mshambuliaji Nicklas Bendtner, jana alishindwa kufunga breki na kuivaa nguzo.
Bendtener alikuwa akiichezea timu yake
ya Arsenal katika mechi ya Kombe la Capital One dhidi ya Wes Brom Albion.
Bendtner alikuwa akijaribu kuiwahi
krosi ya kiungo Ryo Miyaichi ili aukwamishe mpira wavuni.
Hata hivyo alishindwa, mwisho akaivaa
nguzo hiyo na kulazimika kulala chini kutokana na maumivu.
Kiburudisha zaidi kilikuwa ni
mabadiliko ya mwonekano wake, kwani safari hii Mdenishi huyo alikuwa ameachia
ndevu kwa wingi pamoja na nywele zake, tofauti na alivyokuwa akionekana hapo
awali.














0 COMMENTS:
Post a Comment