Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ametua jijini Dar es
Salaam kimya kimya.
Okwi ambaye sasa ni mchezaji wa Etoile du Sahel ambayo ameisusia,
yuko jijini Dar akiendelea na maisha yake ya kawaida.
Rafiki wa Okwi amesema Mganda huyo ametua nchini takribani siku
nne na amekuwa akiishi maisha ya kutotaka kuonekana na watu wengi.
“Amekuja kuwatembelea rafiki zake tu, wala si kwa ajili ya
mazungumzo ya kujiunga na timu nyingine au la,” alisema.
Okwi amesusa kuichezea Etoile inayodaiwa na Simba dola 300,000 za
manunuzi yake ambayo hawakuzitoa.
Mganda huyo aliisusia timu hiyo kwa madai imekuwa haimlipi
mshahara wake kwa zaidi ya miezi miwili.
Kutokana na hali hiyo, Okwi alirejea Uganda na kuendelea na maisha
yake ya kawaida.
0 COMMENTS:
Post a Comment