Mshambuliaji Karim Benzema amelia na mashabiki wa Real Madrid kwamba wamemkatisha tamaa.
Benzema raia wa Ufaransa amesema kumekuwa na tabia ya mashabiki hao kufurahia kila anapotoka.
“Nakata tamaa, najisikia vibaya sana kuona mashabiki wa timu yangu wanafurahia wakiona nimetoka nje,” alisema Benzema.
Hata hivyo, Kocha Carlo Ancelotti amesema mshambuliaji huyo anapaswa kutulia na kujiamini kwa kuwa ana kipaji ana anachohitaji ni utulivu tu.
“Amekuwa akicheza vizuri pembeni ya Ronaldo, atulie na atafanya vizuri tu,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment