September 24, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema hatalitanguliza suala la timu yake kufungwa na Azam FC kama dira.

“Ninachofanya sasa ni kuangalia mchezo wetu na timu ya jeshi (Ruvu Shooting) utakuwa vipi na nini cha kufanya.

“Kama nitaweka mbele suala la sisi kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC kama dira, nitakosea.


“Nimezungumza na wachezaji na kuwaeleza, nimewataka kuwa makini na kuangalia mbele. Kuyaangalia makosa ni jambo la msingi.

“Siku hiyo tulikuwa bora lakini tukashindwa kizitumia nafasi na hilo ndilo tumeliangalia,” alisema Brandts raia wa Uholanzi.
Yanga ilichapwa na Azam kwa mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Katika mechi hiyo, Yanga ilionyesha uwezo mkubwa na kupata nafasi nyingi lakini haikuzitumia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic