IMEFAHAMIKA kuwa Chama cha Soka cha
England (FA) kilikataa uamuzi wa kumpa nafasi Pep Guardiola kuwa kocha wa timu
ya taifa ya England, mwaka jana, badala yake nafasi hiyo akapewa Roy Hodgson.
Taarifa za ndani ya FA zimeeleza kuwa
kutokana na mafanikio aliyokuwa ameyapata Guardiola, 42, alipokuwa akiifundisha
Barcelona ilionekana anaweza kupata nafasi hiyo, lakini mwenyekiti wa zamani wa
FA, David Bernstein alipinga na nafasi hiyo akapewa mzalendo kwa ajili ya
kukuza vipaji vya Uingereza.
Inaelezwa kuwa hatua za awali
zilikuwa zimeanza kufanywa kwa ajili ya kuwasiliana na kocha huyo juu ya nafasi
hiyo, lakini baadaye zoezi likasitishwa na ndipo, Guardiola akatangaza kuwa
atainoa Bayern Munich kuanzia msimu wa 2013-14.
Hodgson, 66, aliteuliwa kuwa kocha wa
England Mei Mosi, mwaka jana na anaitumikia nafasi hiyo mpaka sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment