September 8, 2013



STAA wa Barcelona, Neymar na kiungo wa Chelsea, Ramires waliongoza mashambuzili katika timu yao ya taifa ya Brazil kuifunga Australia mabao 6-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jana jijini Brasilia nchini Brazil.
Brazil ambao ni mabingwa wa Kombe la Mabara walifunga mabao matatu katika kila kipindi cha mchezo huo.
Mabao hayo yalipatikana kupita kwa Jô aliyefunga mawili katika dakika ya 8 na 33, Neymar dakika ya 35, Ramires aliyefunga dakika ya 58, Pato dakika ya 72 na Luis Gustavo dakika ya 83.
Katika mechi hiyo, beki wa pembeni wa Brazil na Real Madrid, Marcelo alishindwa kuendelea na kipindi cha pili cha mchezo huo kutokana na kupata maumivu ya nyama za paja.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic