Rapa maarufu, Kanye West amenunua gari
la kisasa ambalo lina uwezo wa kuzuia mapaparazzi pamoja na watu wanaoweza
kutumia gesi au aside kutaka kumuumiza.
Gari hilo ambalo limetengenezwa nchini
Urusi lina vitasa vyenye umeme ambavyo vinakuwa tatizo kubwa kwa watu wenye
tabia za kudandia au kutaka kuyafungua magari ya watu nyota.
Watu wengi matajiri na maarufu wamekuwa
wakiyanunua magari ya aina hiyo kwa fujo kutokana na kutaka kuwa salama zaidi.
Wengine ambao wamenunua gari kama hilo
ni rapa T.I. pamoja mwigizaji maarufu, Sacha Baron Cohen.
Wahusika katika kampuni inayotegeneza
gari hilo ambalo kiaina linafanana na lile aina ya Hammer, wamesema wasanii na
nyota wa filamu pamoja na watu wenye fedha ambao hawajulikanisa sana wamekuwa
wakiyanunua magari hayo kwa fujo.









0 COMMENTS:
Post a Comment