Leo Messi ameonyesha wazi kutofurahia mfumo wa kocha wake mpya Tata Martino kumtoa uwanjani kabla ya dakika 90 kwisha.
Martino maarufu kama Tata alifanya hivyo kwa mara ya pili wakati Barcelona ikiivaa Real Sociedad katika mechi ya La Liga.
Kocha huyo alimtoa Messi katika dakika ya 81 na nafasi yake kuchukuliwa na Sergi Roberto, hali ambayo ilichukuliwa kama kitu kibaya.
Messi alitoka akiwa ameinamisha kichwa na kupita bila ya kumpa mkono Tata wakati Neymar alipotelewa hakuonekana kukasirika sana na badala yake alitoa mkono na kumpa kocha huyo.
Tata ametangaza kutaka kuwaona wachezaji wake wakicheza kwa kupokezana kadri itakavyowezeakan, lakini ameeleza wazi kwamba atajihidi asimbadilishe Messi zaidi ya mara tano kwa msimu.








0 COMMENTS:
Post a Comment