Wakati timu yake ikichezea kichapo cha mabao 3-1,
kiungo mshambuliaji wa Al-Markhiya Sports Club, Mwinyi Kazimoto alifunga bao la
kufutia machozi, likiwa ni bao lake la nne klabuni hapo.
Nyota ya Kazimoto inaonekana kuendelea kung’aa
akiwa huko akicheza soka la kulipwa, alijiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi
Daraja la Pili msimu huu akitokea kwenye kikosi cha Simba.
Mwakilishi wa klabu hiyo nchini, Saleh Afif
alisema timu yake hiyo ilikutana na kipigo hicho cha kwanza wikiendi iliyopita
katika mchezo wa kirafiki kutoka kwa Al Arabi inayoshiriki Ligi Kuu ya Qatar.
Afif alisema wakati timu hiyo inakutana na kipigo
hicho, kiungo huyo alipachika bao kwa shuti kali alilopiga nje ya 18 na
kumfunga kipa wa timu hiyo, Rajab Chaube kutoka Zanzibar.
“Hilo ni bao la nne kuifungia timu yake tangu
ajiunge na klabu hiyo. Mabao mengi aliyofunga ni ya aina moja, mashuti makali,”
alisema Afif.
0 COMMENTS:
Post a Comment