Kocha wa Makipa wa Yanga, Razack Siwa,
tayari amehakikishiwa kupewa nyumba ya kifahari na usafiri wa ndani iwapo
atajiunga na Mjees FC ya nchini Oman.
Akizungumza na Championi Jumatano, Siwa
ambaye ni raia wa Kenya, alisema amekwishaahidiwa kupata nyumba ya kifahari
ambayo atakuwa akiishi yeye na familia yake kwa kipindi chote atakachokuwepo
katika klabu hiyo.
Alisema pia tayari ameshahakikishiwa
usafiri wa nguvu atakaokuwa akiutumia ndani ya nchi hiyo kwa ajili ya kurahisisha
masuala madogomadogo kama mitoko na mengineyo.
“Wameahidi kunipa nyumba ya kifahari na
usafiri wa nguvu utakaokuwa unanizungusha mimi na familia yangu kwenda
mazoezini au katika mizunguko binafsi na nimekubaliana nao kuhusu hilo,
ninachosubiri ni malipo.
“Hao jamaa wameniambia wanakaa kikao
kujadili mshahara ambao ninautaka, wamefikia pazuri na siyo muda sana
nitaondoka hapa Yanga,” alisema Siwa.







0 COMMENTS:
Post a Comment