![]() |
| Azam FC wakishangilia moja ya mabao yao dhidi ya Yanga leo. |
FULL TIME
Dk 90, Joseph Kimwaga aliyeingia kuchukua nafasi ya Farid Mussa anaipatia Azam FC bao la tatu baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 na Barthes kuteleza.
![]() |
| ...Patashika wakati wa mechi hiyo. |
![]() |
| ...Didier Kavumbagu kazini. |
Dk 69, Kipre aliyeingia kuchukua nafasi ya Umony anaisawazishia Azam FC kwa mkwaju wa penalti baada ya beki wa Yanga kunawa
Dk 65, Kiiza aliyeingia kuchukua nafasi ya Tegete anaifungia Yanga bao la pili
![]() |
| Hamis Kiiza akishangilia baada ya kuifungia Yanga bao la pili. |
KIPINDI CHA PILI:
John Bocco amefunga bao katika sekunde ya 38 na kuipa Azam FC uongozi dhidi ya Yanga.
Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa leo, Bocco alifunga bao hilo mara tu baada ya kuanza kwa mechi hiyo.
Bao hilo la Bocco lilisababisha Yanga kucharuka na kulishambulia mfululizo lango la Azam FC.
Yanga walipoteza takribani nafasi nne za wazi na wangeweza kufunga kama wangekuwa makini zaidi.
Mipira ya Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima iligonga mara mbili mtambaa wa panya wa lango la Azam FC.
Kuanzia dakika ya 35, Azam FC ilionekana kupoteza mwelekeo zaidi na wachezaji wake walilazimika kucheza faulo nyingi ili kuwazuia Yanga.
Timu hizo zilikwenda mapumziko Azam Fc ikiwa inaongoza kwa bao moja.
![]() |
| Kocha wa Yanga, Ernie Brandts akipoza koo. |
![]() |
| Benchi la Azam FC. |
![]() |
| Kikosi cha Azam FC kilichoanza leo. |
![]() |
| Kikosi cha Yanga kilichoanza mtanange wa leo. |
![]() |
| Mashabiki wa Azam FC. |
![]() | |
| Jerry Tegete (katikati) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Azam. |
![]() | ||||
| Mashabiki wa Yanga SC. |



















0 COMMENTS:
Post a Comment