Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jana (Septemba 21 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 123,971,000.
Watazamaji 21,936 ndiyo waliokata
tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 32 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika
kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa
sh. 30,064,741.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
18,910,830.51.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 15,287,156.92, tiketi sh. 3,145,790, gharama za mechi
sh. 9,172,294.15, Kamati ya Ligi sh. 9,172,294.15, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 4,586,147.08 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 3,567,003.28.







0 COMMENTS:
Post a Comment