Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa jana (Septemba 14 mwaka huu) katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 95,080,000.
Watazamaji 16,507 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo namba 15 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa
wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa
sh. 23,018,077.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
14,503,728.81.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 11,704,107.18, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi
sh. 7,022,464.31, Kamati ya Ligi sh. 7,022,464.31, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 3,511,232.15 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 2,730,958.34.







0 COMMENTS:
Post a Comment