Beki wa
kati wa Simba raia wa Burundi, Gilbert Kaze ameshangazwa na soka lililoonyeshwa
na Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na kufika mbali akidai kuwa
inao uwezo wa kutwaa ubingwa kama itaendelea na mwendo mzuri.
Kaze
ambaye ametua Simba hivi karibuni, akitokea Vital’O ya Burundi na kusaini
mkataba wa miaka miwili, amesema kuwa katika mechi tano za ligi hizo hajaona
timu iliyoonyesha ushindani mkali kama Mbeya City ambayo imepanda daraja mwaka
huu.
“Simba
tumecheza mechi tano za ligi mpaka sasa, nimefurahishwa na kiwango cha Mbeya
City walichokionyesha tulipocheza nao.
“Ninaamini
kama mechi zote wakiendelea kucheza jinsi walivyocheza na sisi, basi wataifunga
kila timu watakayocheza nayo ikiwezekana hata kutwaa ubingwa, timu yao inaundwa
na vijana wengi wenye kasi,” alisema Kaze.







0 COMMENTS:
Post a Comment